1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika yakabiliwa na uhaba wa maji

Aboubakary Jumaa Liongo26 Novemba 2010

Shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP limesema nchi nyingi barani Afrika, zitashindwa kufikia malengo ya milenia ya umoja huo ya kupata maji safi na huduma ya maji taka.

https://p.dw.com/p/QJDQ

Katika taarifa yake kufuatia utafiti iliyoufanya shirika la Umoja wa Mataifa limesema ni nchi nane tu zilizo katika nafasi nzuri ya kufikia kwa malengo hayo ambazo ni pamoja na Algeria, Moroko, Libya, Misri, Afrika Kusini, Angola na Botswana.

Nchi hizo zinaonekana kufikia lengo la kupunguza kwa takriban nusu nzima idadi ya watu na uwezo wa kupata huduma za msingi za maji safi na maji taka ifikapo mwaka 2015.

Mkurugenzi mtandaji wa UNEP Achim Steiner amesema tatito la uhaba wa maji barani Afrika linachangiwa na kuongeza kwa idadi kubwa ya watu, matatizo ya uchumi wa kijamii na madhara ya mabadiliko ya halai ya hewa.