1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aghanistan na kashfa ya fedha toka Iran.

Halima Nyanza(ZPR)26 Oktoba 2010

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amekiri kwamba ofisi yake imepokea fedha taslimu kutoka Iran.

https://p.dw.com/p/PnyO
Rais wa Afghanistan Hamid Karzai.Picha: AP

Amesema serikali ya Iran imekuwa ikikabidhi kiasi cha hadi Euro milioni 700 mara mbili kwa mwaka, kwa kile alichokiita ''msaada'' na ''gharama maalumu'', na kusisitiza kuwa fedha hizo zimetolewa kwa njia ya uwazi.

No Flash Iran Atom Präsident Mahmud Ahmadinedschad
Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad.Picha: AP

Rais wa Afghanistan ameyasema hayo, alipokuwa akijibu ripoti iliyochapishwa na gazeti la New York Times kuhusiana na fedha hizo.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, Philip Crowley amewaambia waandishi wa habari kwamba nchi yake bado ina mashaka na hatua hiyo ya Iran ya kuipatia fedha Afghanistan.