1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ahadi za mwenyekiti wa SPD Hessen

5 Machi 2008

Mwenyekiti wa chama cha SPD katika mkoa wa Hessen ataka kuunda serikali ya muungano ikivumiliwa na chama cha mrengo wa shoto-Links.Je, avunja mwiko ?

https://p.dw.com/p/DIKk

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo, wametuwama zaidi juu ya mada moja -kuvunja ahadi kwa Bibi Ypsilanti-mwenyekiti wa chama cha SPD mkoani Hessen.Kwani, siku moja tu baada ya Halmashauri kuu ya chama chake kuidhinisha ushirikiano na chama cha mrengo wa shoto kabisa cha LINKSPARTEI katika daraja ya kimkoa ,alianza kufunua kawa alikua na azma gani moyoni:Alitangaza ana azma ya kuunda serikali ya muungano na chama cha kijani isio na wingi bungeni ikivumiliwa na chama cha mrengo wa shoto cha Linkspartei.Isitoshe, ikibidi hata yutayari achaguliwe waziri-mkuu wa mkoa wa Hesse kwa msaada wa kura za chama hicho cha linkspartei. Aliapa kwa wapiga-kura hapo kabla ya uchaguzi kwamba hangefanya hivyo.Je, sasa amevunja ahadi yake ? Hilo ndilo swali hapa:

Gazeti la NEUE DEUTSCHLAND linalochapishwa Berlin laandika:

►◄

"Chama cha SPD mkoani Hesse kinabidi kuamua ama kuvunja ahadi kama wapinzani wake wa kisiasa wanavyokishtumu kuwa na mafungamano yasiofahamika na chama cha mrengo wa shoto kabisa au kuwaendea kinyume wapigakura wake. Au amvumilie waziri mkuu wa hadi sasa Roland Koch kubakia madarakani ingawa alikua na turufu mkononi kuumaliza utawala wake na hivyo binafsi kuadhibiwa na wenzake chamani.Kwani, uongozi wa chama-taifa mjini Berlin umejitoa na mapema kubeba jukumu hilo."

Ama gazeti la kibiashara litokalo mjini Dusseldorf-Handelsblatt laandika:

"Ukiweka kando ahadi za uchaguzi na -kuvunja ahadi hizo,kutangaza mwenyekiti wa chama cha SPD mkoani Hesse bibi Andrea Ypsilanti kushirikiana na chama cha mrengo wa shoto cha linkspartei ni hatua ya kihistoria.Kwa mara ya kwanza chama cha SPD chaungama kwamba mpasuko chamani kati ya wapinzani wa mageuzi na walioshindwa katika kukiweka chama katika mkondo wa kimambo-leo si jambo la kupita tu bali la kuselelea."

Gazeti laongeza:

"Kwa mara ya kwanza chama hiki klinaingia katika enzi ya mfumo wa vyama 5 kwa kufungua mlango wa uwezekano wa muundo wa serikali ya muungano wa vyama vya mrengo wa shoto-wekundu-kwa wekundu na walinzi wa mazingira kijani.na licha ya viapo vya kutofunga ndoa ya aina hiyo mfumo huo unafungua njia ya kuigwa hata kitaifa.Mtu aweza kwahivyo kusema :chama cha SPD kinautambua sasa ukweli wa mabo."

Hata gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU laonesha kuelewa uwezekano wa ndoa ya kama hiyo:

Laandika:

"Chama cha SPD mkoani Hessen hakijakosea kikiarifu kwamba katika muungano na chama kingine kingebidi kuvunja ahadi nyengine kutokana na kutoafikiana na maazimio.Anaezungumzia uadilifu na uaminifu katika siasa na kuzitoa mhanga ahadi zake katika kampeni za uchaguzi ili huyo anyamaze kimya.Kwani, mfumo mpya wa muungano wa vyama katika magharibi mwa Ujerumani,si uhalifu.Labda yawezekana unajaribiwa mapema kuliko wakati wake kufika na hii huenda ukabainika ni kosa."

Mwishoe,gazeti la MÄRKISCHE ALLGEMEINE kutoka Potsdam lina maoni tofauti kabisa na labainisha wazi maoni hayo.

"Ikiwa mtu asema mambo yasio ya kweli,basi huwa hapo anasema uwongo.Ikiwa mwenyekiti wa chama cha SPD mkoani Hessen anaahidi kitu kingine na baada ya uchaguzi anafanya kingine , basi amefanya kutokana na hisia za jukumu lake alilobeba kwa jamii .

Hivyo ndivyo anavyojitetea.Na sio kwa manufaa yake binafsi.Yamkini ni kweli na kitendo chake hicho kikaja kuingia katika dafutari za historia ya siasa za nchi hii.Hatahivyo, ni vigumu mtu kutofanya dhihaka juu ya kisa hiki cha uvunjaji ahadi aliyotoa mwenyekiti wa chama."