1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aidha Mbeki au Zuma kuongoza ANC Afrika Kusini

18 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cd0l

POLOKWANE

Chama cha Ukombozi wa Afrika Kusini cha ANC leo kinapiga kura kuchaguwa uongozi wa chama hicho ambapo yumkini ukawa ni mwisho wa Rais Thabo Mbeki kuwa na udhibiti wa chama hicho tawala.

Iwapo mpizani wake Jacob Zuma ambaye ni naibu wake wa chama atashinda takriban atakuwa na uhakika kabisa wa kuwa rais wa Afrika Kusini wakati Mbeki inapobidi an’gatuke katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2009.

Mvutano na mabishano ya ndani ya chama hicho juu ya sifa za wajumbe wanaostahiki kupiga kura,taratibu za kupiga kura na kurepotiwa kuwepo kwa mbinu chafu kutoka pande zote mbili ile inayomuunga mkono Mbeki na ile inayomuunga mkono Zuma kumepelekea kuahirishwa kwa uchaguzi huo uliokuwa awali umepangwa kufanyika hapo Jumapili.

Mbeki alimtimuwa Zuma kwenye wadhifa wa makamo wa rais hapo mwaka 2005 baada ya kuibuka kwa madai ya rushwa dhidi yake hata hivyo inatabiriwa kwamba Zuma atashinda uchaguzi huo licha ya kukabiliwa na madai hayo pamoja na kuwahi kukumbwa na kashfa ya kumbaka mwanamke mwenye virusi ya UKIMWI.