1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ajali ya meli ya anasa karibu na fukwe za Italy

Oumilkher Hamidou16 Januari 2012

Ajali ya meli ya fakhari ya kitaliana "Costa Concordia" katika fukwe za Italy,kuteremshiwa Ufaransa alama yake moja na uchaguzi mkuu nchini Misri .ndizo mada kuu magazetini

https://p.dw.com/p/13kFy
Abiria wanaokolewa toka meli ya Anasa ya Costa Concordia
Abiria wanaokolewa toka meli ya Anasa ya Costa ConcordiaPicha: picture-alliance/dpa

Tuanzie lakini na kitisho cha kuanza kuzama meli ya anaza ya Italy iliyogonga mwamba karibu na fukkwe za nchini hiyo.Gazeti la "Kieler Nachrichten" linalinganisha na ajali zilizowahi kutokea zamani na kuandika:Kama ilivyotokea mwaka 1912, na safari hii pia mengi yanaonyesha kwamba uzembe wa binaadam ndio chanzo cha ajali hii na sio mitambo iliyokongaa au kazi mbaya.Meli ya anasa ya Titanic ilikuwa mpya,kama ilivyo hii ya Costa Concordia.Katika ajali ya Titanic,nahodha alizama na meli yake kwa hivyo alichokifanya na kusababisha meli kuzama anakijua huko huko aliko kaburini.Hii leo hali ni nyengine.Suala,kwanini Costa Concordia imegonga mwamba karibu na fukwe za Giglio halitakawia kujibiwa."Kinasa sauti" au kama kinavyojulikana kitaalam "Blackbox"kitakaposikilizwa tu,wachunguzi wataelezea nini kilijiri dakika 60 kabla ya ajali hiyo kutokea.Kibweta hicho kwa bahati nzuri hakijaharibika."

Gazeti la "Der neue Tag" linaandika:"Safari za meli za anasa ni biashara nono ya mabilioni ya Euro.Ndio maana,gharama zinapunguzwa ili faida ipate kuwa kubwa.Ikilazimika basi idadi ya wafanyakazi inapunguzwa, au mchoro mwekundu unapita katika idadi ya wanaopatiwa mafunzo.Pengine zitapita wiki kadhaa hadi chanzo cha ajali kitakapojulikana.Si hasha lakini kwamba sababu ya yaliyotokea katika bahari ya kati inajulikana tokea sasa.

Nembo ya taasisi ya Standard & Poor
Nembo ya taasisi ya Standard & PoorPicha: picture-alliance/dpa

Mada yetu ya pili magazeti ni inahusu kuteremshiwa Ufaransa alama yake moja kati ya tatu za uwezo wake wa kulipa madeni.Gazeti la "Frankfurter Allgemeine Zeitung" linaandika: Juhudi za kuifanyia marekebisho kanda ya Euro zitakuwa ngumu baada ya nchi nyingi wanachama kuteremshiwa alama za uweo wao wa kulipa madeni.Na kisa hicho kinazidisha mvutano katika uhusiano kati ya Ujerumani na Ufaransa.Ujerumani inajikuta katika hali ya kulazimika kuiokoa jahazi nzima ya Euro(jambo ambalo linapindukia uwezo wake).Na kila wakati Sarkozy anaonekana kama hana jengine isipokuwa kufuata msimamo wa Ujerumani.Mnamo wiki za hivi karibuni rais Sarkozy amekuwa kila wakati akiisifu Ujerumani kuwa ndio mfano mwema wa kufuatwa na Ufaransa-hiyo ikiwa ni mbinu hatari ya uchaguzi katika nchi ambayo daima inajifakharisha.Kwa kubebeshwa jukumu la mshika bendera,unakuwa pia mzigo kwa Ujerumani.

Mmoja wa waandamanaji katika uwanja wa Tahrir nchini Misiri
Mmoja wa waandamaanji katika uwanja wa TahrirPicha: dapd

Mada yetu ya mwisho magazetini inahusu jinsi uchaguzi ulivyofanyika nchini Misri.Gazeti la "FInacial Times Deutschland" linaandika: Misri imefeli mtihani wake wa kwanza kuelekea Demokrasia.Utaratibu jumla ya uchaguzi haukuwa wa haki.Majenerali hawaonyeshi dalili ya kuwaachia wawakilishi wa wananchi washiriki katika uchaguzi wa rais uliopangwa kuitishwa msimu wa kiangazi ujao.Wachache tu nchini Misri ndio wanaouamini utaratibu wa kuleta demokrasi unaosimamiwa na wanajeshi.Jumuia ya kimataifa,na hasa Marekani ambayo ndio mfadhili mkubwa wa wanajeshi ,inakosoa kuvunjwa vibaya sana haki za binaadam,lakini wakati huo huo wanaiunga mkono serikali kwa lengo la kupatikana utulivu.Hoja kama zile zilizotolewa mwaka mmoja uliopita,kabla ya mapöinduzi dhidi ya Mubarak.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlnadspresse

Mhariri: Yusuf Saumu