1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ajali ya ndege

18 Julai 2007

Hadi sasa wsatu 189 wamethibitika wameuwawa katika ajali ya ndege iliozuka jana jioni nchini Brazil.

https://p.dw.com/p/CHk9

Katika ajali ya ndege ya hapo jana huko sao Paulo,Brazil ambamo watu hadi 200 wanahofiwa kuuwawa,rubani wa ndege hiyo-Airbus chapa 320, yasemekana alijaribu kutaka kuruka tena ndege hiyo baada ya kutua.Idadi inayojulikana ya waliouwawa imefikia 189 na yamkini ikapanda .

Uwsanja wa ndege wa Congonhas,mjini Sao Paulo, Brazil ukikosolewa mno kwa hitilafu zake nyingi kwa kutua ndege.Ndege iliopatwa na ajali hapo jana iliteleza na kujigonga na jumba la ghala ya mizigo na kuendelea hado barabara kuu ya magari iliposimama ikiwaka moto mbele ya kituo cha mafuta ya petroli.

Siku 2 tu kabla kisa cha jana jioni,ndege mbili tofauti nah ii zilichomoka nje ya njia zake za kupita baada ya kutua zilizoroa maji ya mvua .

Uwsanja huu wa kutua ndege unaangaliwa na marubani kuwa ni mfupi kwa ndege kubwa na umezungukwa na mtaa wa majumba ya wakaazi wengi.

Kwa muujibu wa taarifa za hivi punde, rubani wa ndege iliopatwa jana na ajali aliposhindwa kutua sawa sawa,alifanya jaribio la kuruka tena .Hapo tena, ndege hii ikitoka Port Alegre, kusini mwa Brazil, ikielekea Sao Paulo,ikavuka ua wa uwanja wa ndege na kuwasili barabara kuu ya magari na hapo ikajigonga na kituo cha mafuta na jengo la shirika la ndege la TAM na kuripuka moto.Hakujakua na nafasi ya abiria yoyote kunusurika na maisha.

Ajali hii ilitokea muda mfupi kabla ya saa moja ya usiku jana .Kikosi cha wazima moto kilifaulu baadae kuudhibiti moto uliowaka na kiasi cha watu 15 waliuwawa ardhini au nje ya ndege hiyo.

Chanzo hasa cha ajali hii hakifahamiki bado.Lakini, juzi jumatatu,ndege moja ya shirika la Brazil la PANTANAL iliteleza baada ya kutua na kunasa.

Uwanja huu wa kurukia ndege na kutua, ulifunguliwa upya kwa safari za ndege siku chache tu zilizopita baada ya lami mpya kutandazwa .Yasemekana wakuu wa uwanja, waliruhusu kuanza tena misafara japo kuwa njia ya kutiririkia maji yanayosheheni uwanjani haikutengezwa.Kazi hiyo ilikua ianze baada ya wiki 2 zijazo.Mvua ikinyesha wakati ajali hii ilipozuka.Kwa muujibu wa shahidi mmoja,kulikuwapo kidimbwi cha maji katika njia ya kutua ndege.

Hii ndio ajali mbaya kabisa ya safari za ndege nchini Brazil, tangu ile ya Septemba,mwaka jana pale abiria 154 walipouwawa katika mgongano kati ya ndege ya shirika la Brazil GOL na ile ya shirika la Marekani Firmjet.

Rais Lula da Silva wa Brazil, ametangaza maombolezi ya siku 3 kwa taifa zima na aliitisha kikao cha dharura cha Baraza lake la mawaziri.