1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al Saadi Gaddafi kujisalimisha

1 Septemba 2011

Waasi nchini Libya wanasema kuwa mmojawapo ya wanawe wa kiume kiongozi aliyetimuliwa Muammar Gaddafi, Al Saadi amekuwa akijaribu kujadiliana nao masharti ya kujisalimisha.

https://p.dw.com/p/12RMk
Mwanawe Muammer Gaddafi, Al-Saadi Gadhafi.Picha: AP

Mwanawe maarufu Gaddafi, Seif al Islam ameapa kupigana hadi kufa kwake.

Libyen Gaddafi Sohn Saif al-Islam in Tripolis
Seif al-Islam GaddafiPicha: Dapd

Baraza la kitaifa la waasi nchini humo limewapa wafuasi wanaomtii Gaddafi muda hadi Jumamosi kujisalimisha, likisema kuwa litalazimika kutumia nguvu za kijeshi hapo baadaye.

Mashambulio ya waasi yanaendelea katika maeneo makuu yanayodhibitiwa na Gaddafi kama mji alikozaliwa kiongozi huyo, Sirte.

Uongozi mpya Libya umeuambia Umoja wa mataifa hautaki jeshi la kimataifa au waangalizi kutumwa nchini humo, punde mzozo huo utakapokamilika. Hata hivyo mjumbe maalumu wa Umoja huo, Ian Martin, amesema kuwa watahitaji msaada.

Libyen Tripolis Rebellen
Picha: dapd

Martin alisema kuwa wamesisitiza haja ya ushauri wa Umoja wa mataifa katika maeneo ya haki katika serikali ya mpito, masuala magumu waasi hao watakayokabiliana nayo katika kuweka sawa sheria, uwajibikaji katika sheria na kwa wale waliokiuka haki za binaadamu na haja ya maridhiano ya kitaifa.

Ufaransa imewakaribisha viongozi duniani mjini Paris hii leo, kujadili jitihada za kuijenga upya Libya.

Mwandishi: Maryam Abdalla/afpe, rtre, dpae
Mhariri: Charo, Josephat.