1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al-Shabaab waukimbia mji wa Mogadishu

6 Agosti 2011

Rais Sharif Sheikh Ahmed wa Somalia ameahidi kwamba majeshi yake yatarejesha amani na utengamano katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu, baada ya wapiganaji wa al-Shabaab kuukimbia mji huo.

https://p.dw.com/p/12CFw
Wapiganaji wa kundi la al-Shabaab wakisafiri katika gari ya pickup nchini Somalia.Picha: AP

Rais Sharif Sheikh Ahmed wa Somalia ameahidi kwamba majeshi yake yatarejesha amani na utengemano katika mji wa Mogadishu baada ya wapiganaji wa al-Shabaab kurejea nyuma na kuondoka kutoka mji mkuu huo alfajiri ya leo, baada ya kujiri masaa kadhaa ya mapigano. Aliuwambia mkutano wa waandishi wa habari katika kasri yake inayolindwa vikali kwamba ni wakati sasa wa kuvuna matunda ya amani. Rais huyo, ambaye mwenyewe alikuwa mwanachama wa kikundi cha Kiislamu ambacho kilidhibiti sehemu za nchi hiyo hapo zamani, alitoa mwito kwa raia kuwaariffu wakuu wa serekali juu ya harakati zozote za wapiganaji wa Kiislamu wanaojificha katika mji huo.

Somalia Scheich Scharif Ahmed
Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, wakati huo akiwa kiongozi wa baraza la mahakama za Kiislamu nchini Somalia.Picha: AP

Waziri mkuu wa Somalia, Abdiweli Mohamed Ali, alihakikisha kwamba mji huo ulikuwa unadhibitiwa kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka na serekali yake ilio dhaifu, na kwamba wataendelea kuwafyeka al-Shabaab katika mikoa yote.