1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Leo ni kumbukumbu ya miaka 56 ya Ampelmännchen Ujerumani

13 Oktoba 2017

Ni ubunifu wa Karl Peglau aliyebuni taa hizo za barabarani zenye picha ya mwanaume mfupi akiongoza watembea kwa miguu katika miji mingi duniani

https://p.dw.com/p/2lnuI
Ampelmännchen aus aller Welt EINSCHRÄNKUNG
Picha: ampelmann.de

Ukipita katika mitaa mbalimbali mjini Bonn, Berlin na kwingineko Ujerumani, kama katika nchi nyengine utashuhudia taa zinazowaongoza watembea kwa miguu kuvuka katika barabara. Lakini jee unajua zilibuniwa Ujerumani ?

Taa hizo zina picha ya  mwanaume mfupi  akiongoza watembea kwa miguu.

Akitokea mwanaume mwenye rangi nyekundu, basi si salama na akitokea wa rangi ya kijani, hapo ni salama kuvuka. Kwa lugha ya Kijerumani, Ampelmännchen yaani mtu wa taa, alama ambayo leo imetimiza miaka 56 tangu kubuniwa kwake.

 Hayo yote yalibuniwa  Oktoba 13 mwaka 1961 na  Karl Peglau ambaye alibuni Ampelmänchen  kwa ajili ya watembea kwa miguu. Ampelmänchen   au mtu wa taa ameendelea kuwa ni alama kubwa ya utambulisho wa miji mingi Ujerumani.

 Wazo la Peglau lilivyozaliwa

Tarehe kama ya leo Peglau, alikutana na tume ya usalama barabarani ya Berlin mashariki, ili kuwasilisha wazo lake la kupunguza ajali za barabarani.

Utafiti wake ulibaini kuwa ajali za barabarani zinaweza kuzuiwa iwapo watembea kwa miguu watakuwa na taa zao badala ya kutegemea zinazotumiwa na madereva.

Belgien | Ampelmänner und Ampelfrauen in Brüssel
Picha: Getty Images/AFP/N. Maeterlinck

Karl alishauri kuwepo kwa alama mbili, mwanaume mwenye rangi ya kijani akimaanisha ni salama kuvuka na mwanaume mwenye rangi nyekundu aliyenyoosha mikono akimaanisha si salama kuvuka. Ombi lake lilikubaliwa na likafanya vyema katika kupunguza ajali.

Baada ya ukuta wa Berlin kuanguka, serikali ilitaka kuziondoa alama hizo lakini kundi la watu wa Ujerumani Mashariki walianzisha kampeni ya ´muokoe Ampelmännchen.´ 

Mtu wa taa aliendelea kutumika na ni alama kubwa inayoitambulisha Ujerumani mpaka sasa. Heri ya miaka 56 Ampelmännchen kitambulisho cha usalama barabarani.

Mwandishi: Florence Majani(Internet source including google, Welt N24)

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahmann