1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Algeria yabanwa na Angola katika mechi ya ufunguzi AFCON

16 Januari 2024

Timu ya taifa ya Algeria imetoka sare ya 1-1 na Angola katika mechi yao ya ufunguzi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON.

https://p.dw.com/p/4bJ2d
Fußball | Afrika Cup | Algerien vs Angola
Picha: Kenzo Tribouillard/AFP/Getty Images

Penalti ya kipindi cha pili iliyofungwa na Agostino Mabululu iliwanyima Algeria ushindi katika mechi yao ya kwanza.

Algeria, ambao ni mabingwa wa AFCON wa mwaka 2019 walitupwa nje katika hatua ya makundi miaka miwili iliyopita, na sasa imeungana na miamba Nigeria, Misri, Ghana na Cameroon ambao wameshindwa kutamba katika mechi zao za ufunguzi.

Jana, Cameroon pia ilitoka sare ya 1-1 na Guinea. Michuano hiyo inaendelea tena leo ambapo Burkina Faso itacheza na Mauritania, Tunisia itachuana na Namibia na baadaye usiku, itakuwa ni zamu ya Mali kukabana koo na Afrika Kusini.