1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Algeria yakosoa mpnago wa UN wa kufanya uchunguzi kuhusu shambulio la Bomu la mwaka jana

16 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CqDB

ALGIERS:

Waziri Mkuu wa Algeria, amekosoa uamuzi wa Umoja wa Mataifa wa kuunda tume huru kuhusu shambulio la mabomu nchini Algeria la mwezi jana mjini Algiers ambapo, miongoni mwa wengine, watumishi wa Umoja wa Mataifa 17 waliuawa. Jumatatu mkuu wa Umoja wa Mataifa-Ban Ki-moon alisema kuwa atateua jopo la wataalamu kutoka nje ya mfumo wa Umoja wa Mataifa ili kufanya uchunguzi wa shambulio hilo.Maafisa wa Umoja wa Mataifa walisema wataomba ushrikiano wa karibu na wakuu wa Algeria.Kwa uchache watu 41 waliuliwa katika milipuko ya mabomu miwili,ambayo ilidaiwa kutegwa na tawi la Algeria la mtandao wa kundi la kigaidi la Al-Qaida.