1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Algeria yapitisha sheria ya kupandisha kodi

Caro Robi
23 Novemba 2016

Serikali ya Algeria imepitisha mswada wa kubana matumizi unaojumuisha kuongezwa kwa kodi na kusimamishwa kwa mishahara ili kukidhi kushuka sana kwa mapato yapatikanayo kutokana na mauzo ya gesi.

https://p.dw.com/p/2T6ti
Parlament Algerien
Picha: Reuters/R. Boudina

Wengi wa wabunge wa chama tawala  Algeria waliuidhinisha mswada huo hapo jana huku wabunge wa upinzani wakisusia kura hiyo.

Mohamed Djemai, mbunge wa chama tawala cha National Liberation Front, amesema ameunga mkono mswada huo kwani hauathiri mafao ya kimsingi ya kijamii ya Waalgeria, licha ya matatizo ya kiuchumi.

Wanaoupinga mswada huo, wakiwemo walimu na wahudumu wa afya nchini humo, wamepanga kufanya maandamano kuanzia tarehe 27 hadi 29 mwezi huu.

Mabadiliko katika bajeti yatapelekea kuanzishwa kwa kodi mpya na kuongezwa kwa bei za tumbaku, pombe na mafuta.

Wakosoaji wa mswada huo wanaishutumu serikali na matajiri kwa kujilimbikizia mali nyingi, ilhali wananchi wa kawaida wakitaabika na mfumko wa bei.