1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS: Rais wa Ujerumani ziarani barani Afrika

12 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJn

Rais wa Ujerumani Horst Köhler akiwa katika ziara rasmi ya siku mbili nchini Algeria amekutana na rais mwenzake Abdelaziz Bouteflika.Köhler aliefuatana na Waziri wa Misaada ya Maendeleo wa Ujerumani,Heidemarie Wieczorek-Zeul,leo atafungua mkutano unaohusika na ushirikiano kati ya madola fadhila na nchi za Kiafrika.

Rais Köhler anatazamiwa pia kushiriki kwenye mkutano wa Algeria na Ujerumani unaohusika na usalama wa nishati na mabadiliko ya hali ya hewa.Hii ni ziara yake ya nne barani Afrika,tangu kushika madaraka ya urais mwaka 2004.