1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS: Waafrika wanufaike kutokana na malighafi yao

13 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJZ

Rais wa Ujerumani Horst Köhler ametoa mwito wa kuwepo masharti ya kibiashara yenye usawa kwa nchi za Afrika.Amesema,sera lazima zihakikishe kuwa Waafrika wananufaika kutokana na malighafi yao.

Akasema,kwa maoni yake, Algeria haina utajiri wa madini tu,kwani utajiri wake ni vijana wake pamoja na matumaini na ndoto za vijana hao.Ikiwa kutakuwepo ushirikiano kwa mfano katika sekta ya elimu na mafunzo na pia uhuru wa usafiri,basi hapo Ujerumani itaweza kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya Algeria.

Rais Köhler alikuwa akifungua kikao cha Ushirikiano na Afrika katika mji mkuu wa Algeria, Algiers,kama sehemu ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo.Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Misaada ya Maendeleo wa Ujerumani Heidemarie Wieczorek-Zeul na wajumbe wa Kundi la Mataifa Manane yaliyoendelea Kiviwanda(G-8); Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) na mataifa ya Kiafrika.