1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS:Uchaguzi kuendelea kama ilivyopangwa

12 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAb

Waziri Mkuu wa Algeria Abdelaziz Belkhadem anasisitiza kuwa uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa mwezi ujao hata baada ya milipuko kutoka hapo jana mjini Algiers.Watu 24 waliuawa na wengine 222 kujeruhiwa.

Kundi la Al Qaeda la Kaskazini mwa Afrika lilikiri kutekeleza Milipuko hiyo iliyotokea muda mfupi baada ya milipuko kutokea nchini Morocco.Hayo ni kwa mujibu wa taarifa waliyotoa kupitia mtandao.

Taarifa hiyo iliyochapishwa katika mtandao wa Kiislamu unaotumiwa sana na kundi la magaidi la Al Qaeda la Osama b in Laden ilisema kuwa mabomu ya kutegwa garini yalisababisha vifo vya takriban watu 53.

Wakati huohuo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anayapinga vikali mashambulio hayo na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kushirikiana kwa pamoja kukabiliana na ugaidi.Kiongozi huyo anasisitiza kuwa kuna umuhimu wa kupambana na ugaidi unaoathiri maisha ya kawaida ya raia.