1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aliyedengua ndege ya PanAm aachiwa huru

Oumilkher Hamidou20 Agosti 2009

Marekani yalalamika dhidi ya kusamehewa raia wa Libya Mohamed Al Megrahi kwasababu za kiutu

https://p.dw.com/p/JFJP
Abdelbaset al MigrahiPicha: AP

Serikali ya Scottland imeamua kuamuachia huru "kwasababu za kiutu" raia wa Libya" Abdel Basset el Megrahi",aliyehukumiwa kifungo cha maisha kwa kuhusika na kuidengua ndege ya kimarekani chapa PanAM katika anga ya Lockerbie mnamo mwaka 1988.

Akitangaza uamuzi huo, waziri wa sheria wa serikali ya Scottland Kenny MacAskill amesema:

"Uamuzi wangu umetokana na ule ukweli kwamba anakwenda kufa nyumbani.Habari tulizo nazo zinaonyesha amesaliwa na miezi michache tuu ya kuishi.Nnatambua fika kwamba amefanya maovu yaliyokithiri katika ardhi ya Uengereza,maovu ambayo nchi yetu na wananchi wetu hawajawahi kuyashuhudia...lakini nnasema tuna mila zetu kama nchi na kama umma.Tunabidi kuonyesha huruma hata kama yeye hajawahurumia watu 270 waliowawa.

Waziri huyo wa sheria aliyesema hayo wakati wa mkutano pamoja na waandishi habari mjini Edimbourg,ameeleza kwamba Al Megrahi alikua njiani kuelekea uwanja wa ndege wa Glasgow kwa safari ya kurejea nyumbani nchini Libya.

"Mfumo wetu wa sheria unalazimisha mwenye makosa ahukumuwe,lakini ubinaadam pia uzingatiwe-imani yetu inashurutisha hukmu ipitishwe lakini msamaha pia utolewe.

Amesisitiza waziri huyo wa sheria.

Uamuzi wa kumuachia huru Abdelbaset Ali Mohammed Al Megrahi umetangazwa pia na afisa wa ngazi ya juu wa wizara ya ndani ya Libya mjini Tripoli.

Gaddafi auf offiziellem Besuch in Italien
Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi alipokua ziarani nchini ItalyPicha: picture alliance / dpa

Aicha,mke wa Megrahi amesema "furaha yake haina kifani."

Waziri MacAskill amehakikisha hajapitisha uamuzi huo kutokana na shinikizo la kimataifa.

Marekani haijakawia kuelezea masikitiko yake kwa kuachiwa huru Al Megrahi.Familia za wahanga wa kimarekani zinapinga msahama huo na kudai Al Megrahi atumikie hadi mwisho adhabu aliyohukumiwa.

Frank Duggan,ambae ni mwenyekiti wa jumuia ya wahanga wa shambulio la ndege ya Pan AM,alisema tangu asubuhi tunanukuu:""hata kama yuko mahtuti,anastahiki kumaliza maisha yake jela."Mwisho wa kumnukuu.

Megrahi alihukumiwa kifungo cha maisha kikishurutishwa na kipindi cha miaka 27 bila ya msamaha kwa kuhusika na shambulio dhidi ya Boengi chapa 747 ya shirika la ndege la Marekani Pan Am,iliyoripuka December 21 mwaka 1988 katika anga ya mji mdogo wa Lockerbie huko Scottland na kuangamaza maisha ya watu 270-wengi wao ni raia wa Marekani.

Libya,ambayo uhusiano wake na nchi za magharibi umerejea upya kuwa mzuri tangu ilipotangaza kuteketeza silaha za maangamizi mnamo mwaka 2003 na kukubali kuwalipa fidia familia za wahanga wa shambulio hilo,ilionya kwamba Uengereza ingeweza kukumbwa na madhara ya kiuchumi kama Megrahi asingeachiwa huru.

Mwandishi.Hamidou,Oummlikheir /afp

Mhariri:Abdul-Rahman