1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Aliyekuwa waziri wa elimu ya juu nchini Kenya awasili Uholanzi

4 Novemba 2010

Aliyekuwa waziri wa elimu ya juu nchini Kenya William Rutto yuko mjini the Hague, Uholanzi kukutana na mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, Luis Moreno Ocampo.

https://p.dw.com/p/PyRU
Luis Moreno Ocampo wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICCPicha: dpa - Fotoreport

Bwana Rutto aliondoka jana mjini Nairobi akiwa ameandamana na mbunge wa Belgut, Charles Keter. Mawakili wake walimtangulia, kuandaa mazungumzo ya kina na muhimu na Ocampo. Mwandishi wetu Alfred Kiti na ripoti kamili kutoka Nairobi.

Mwandishi: Alfred Kiti

Mhariri: Josephat Charo