1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

All-Africa Games Algiers-riadha yatia fora:

Ramadhan Ali19 Julai 2007

Waethiopia na wakenya wameanza kutamba katika medani ya riadha pale bunduki zilipolia jana kwa mashindano hayo.wanariadha wengi wanajinoa kwa mashinda no ya dunia huko Osaka,japan mwezi ujao.

https://p.dw.com/p/CHbe

Mashindano ya riadha yameanza kwa kishindo katika All-Africa Games huku Kenya na Ethiopia zikiumana.Michezo ya pan-American games nayo yasonga mbele mjini Rio de Jeneiro licha ya msiba wa ajali ya ndege ulioikumba Brazil.Mpambano kati ya timu ya Afrika nay a dunia kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mzee Mandela, yamalizika suluhu mabao 3:3 mjini Cape Town.

Baadhi ya majina ya mastadi wakubwa wa dimba tangu wa enzi hii hata ya zamani yaliteremka jana uwanjani huko Cape Town kwa dakika 90 za mzee Mandela alieadhimisha jana miaka 89 ya siku ya kuzaliwa.

Jogoo la FC Barcelona, Samuel Eto’o kutoka Kamerun,mholanzi –mchezaji bora wa mwaka wa Ulaya- Ruud Gullit na George Weah wa Liberia,mchezaji bora wa dimba wa dunia, walikuwa uwanjani katika changamoto iliomalizika suluhu mabao 3:3.

Beki-mshahara wa Afrika Kusini, Lucas Radebe na mwenzake Mark Fish pamoja na mfaransa Christian Karembu walikuwa pia uwanjani.

Vigelegele na mazumari ya Vuvuzela vilihanikiza uwanjani huko Cape Town ingawa mzee Mandela binafsi hakuweza kuhudhuria.

Mfalme wa dimba wa Brazil-Pele alianzisha dimba hilo.Mastadi tangu wa zamani hata wa sasa walionesha ustadi wsao-akina Hossam Hassan alietia mabao 2 na Ruud Gullit na hata pia Pele wa Afrika-Abedi Pele kutoka Ghana.Kila mmojawao alitia bao.

Mechi hiyo iliochukua biramu la kupinga ubaguzi ilikamilisha siku 2 za tafrija ya FIFA ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa mzee Nelson Mandela.Jana,FIFA ilitoa uanachama wa heshima kwa chama cha mpira cha Makana football Association chama kilichoundwa na wafungwa kama Mandela katika kisiwa cha Robben,nje ya pwani ya Cape Town.

Katika All-Africa Games-michezo ya bara la Afrika mjini Algiers,Algeria, mashindano ya riadha yalianza jana kwa msisimko huku bingwa wa olimpik wa Kenya katika mita 3000 kuruka viunzi Ezekiel Kemboi akishindwa kufua dafu-taji likinyakuliwa n a mkenya mwenzake Willy Komen.Kemboi alibidi kuridhika na medali ya fedha.

Muethiopia Nahom Mesfin aliwatilia wakenya kitumbua chao mchanga alipowapokonya medali ya shaba katika mbio ambazo wakenya huzowa zote tatu.

Bingwa mwengine wa Olimpik-muethiopia Meseret Defar,bingwa pia wa rekodi ya dunia ingawa alishinda mbio za mita 5000,mwenzake Werkitu Ayanu alimaliza 6.

Meserat alitarajia waethiopia wangelizoa medali zote 3.Mwenzake Melkamu alikuja wapili huku medali ya shaba ikichukuliwa na mkenya Sylvia Kibet akitoroka na medali ya shaba.Kemboi na Defar wanajiandaa kwa changamoto za ubingwa wa dunia huko Osaka,Japan mwezi ujao.

Katika changamoto ya mbio fupi za mita 100,mwendambio wa kasi kabisa barani Afrika wakati huu Fasuba Olusoji wa Nigeria alitamba bila ya taabu katika nusu-finali yam bio hizo na inaonesha taji ni lake.

Katika hodhi la kuogolea, mkenya Jason Dunford ametwa medali yake ya 3 ya dhahabu katika mita 200 kipepeo.

Katika Pan American Games-michezo ya bara la Amerika,licha ya msiba wa ajali ya ndege Brazil imeendelea kutamba ikichukua jana medali 2 za dhahabu zote kutoka hodhi la kuogolea.

Cuba nayo ambae rais wake Fidel Castro,hakuna mchezo unaompita kwenye TV, inazidi kuparamia kileleni:Cuba iko nyuma ya Marekani katika orodha ya medali.

Kombe la Asia linasubiri kwa hamu robo-finali mwishoni mwa wiki hii:Australia ina miadi na mabingwa Japan kuania nafasi ya nusu-finali ya na siku ya pili yake hapo jumapili, itakua zamu ya Saudi Arabia kupambana na Uzbekistan.Wasaudi wamepania mara hii kufuta madhambi ya kombe lililopita nchini China,ilipopigwa kumbo duru za kwanza.Japan itadurusu ule mchezo na Australia wa kombe la dunia mwaka jana Ujerumani kujua nini kilienda kombo.

Mwishoe, Tour de France-mbio za baiskeli za Ufaransa, zimegubikwa tena na madhambi ya doping-matumizi ya madawa kutunisha misuli:Nchini Ujerumani,tangu viongozi wa spoti hata wanasiasa wamekaribisha uamuzi wa jana wa vituo 2 vya TV ARD na ZDF kuacha kuripoti juu ya mbio hizo baada ya mjerumani mwengine Patrik Sinkewitz kugunduliwa na madhambi hayo.