1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALSUNGA: Watu 26 wauwawa kwenye ajali ya moto

23 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCPM

Watu 26 wameuwawa leo baada ya moto kuzuka kwenye nyumba ya walemavu magharibi mwa Latvia. Moto huo ulizuka mapema leo mjini Alsunga, yapata kilomita 200 kutoka mji mkuu Riga.

Waokoaji wamefaulu kuwaokoa madarzeni ya watu kutoka jengo lililokuwa likiwaka moto kabla paa lake kuporomoka.

Kilichosababisha moto huo hakijajulikana, lakini waziri anayehusika na mashlahi ya raia nchini Latvia, Dagnija Stake, amesema huenda moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme.