1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amani inawezekana mashariki ya kati anasema rais Bush

Oummilkheir29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUdF

Washington:

Bush amewahakikishia viongozi wa Israel na Palastina Marekani itawajibika kikamilifu katika utaratibu wa amani uliofufuliwa Annapolis..Siku moja baada ya mazungumzo hayo,waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na kiongozi wa utawala wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas walikutana tena na rais Bush katika ikulu ya marekani mjini Washington.Katika mkutano pamoja na waandishi habari,pamoja na waziri mkuu na kiongozi wa utawala wa ndani Mahmoud Abbas,rais Geoirge Bush amesema anaamini amani inaweza kupatikana.

Mjumbe maalum wa pande nne zinazosimamia utaratibu mpya wa amani ya mashariki ya kati,Tony Blair ana maoni sawa na hayo.

“La muhimu zaidi katika mkutano wa Annapolis ni kwamba pamebuniwa utaratibu unaofuata ratiba maalum,yaani mwaka 2008 - sio kuzungumzia baadhi ya masuala-lakini kujaribu kuyapatia ufumbuzi masuala yote kati ya Israel na Palastina.“Wakati huo huo kiongozi wa zamani wa vikosi vya jumuia ya kujihami ya magharibi NATO barani Ulaya,James Jones,ameteuliwa kusimamia mazungumzo ya amani ya mashariki ya kati.Jenerali huyo wa zamani atashirikiana zaidi na wapalastina na waisrael katika masuala ya usalama-amesema hayo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice.