1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amani ya Afghanistan bado ni kitendawili

Josephat Nyiro Charo23 Julai 2013

Ripoti ya Taasisi ya Kimataifa ya ICRS, inasema Afghanistan ina nafasi finyu ya kufikia makubaliano ya amani kati ya serikali na kundi la Taliban baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa kimataifa nchini humo mwaka ujao 2014.

https://p.dw.com/p/19DB8
Ehemalige Taliban-Kämpfer bei Waffen Übergabe in Herat, Afghanistan
Ehemalige Taliban-Kämpfer bei Waffen ÜbergabePicha: picture alliance / AP Photo

Kwa mujibu wa ripoti ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia masuala ya itikadi kali na machafuko ya kisiasa, ICSR, iliyozinduliwa siku ya Jumatatu uwezekano wa kufikia muafaka wa amani na kugawana madaraka nchini humo kufuatia kuondoka kwa wanajeshi hao wanaoongozwa na Marekani ni mdogo mno. Matokeo ya uchunguzi uliofanywa na Taasisi ya Kimataifa kuhusu itikadi kali na machafuko ya kisiasa,ICSR, yameonyesha wazi dhahiri shahiri kuwa kumetokea makosa makubwa katika juhudi za kidiplomasia zilizofanywa na Marekani ambazo zimeshindwa kabisa kuweka mazingira yanayohitajika kuhakikisha mageuzi shwari ya utawala wa kisiasa wa mpito kufikia taifa huru la Afghanistan.

Ripoti hiyo inaeleza kwa kina matokeo ya uchunguzi juu ya jitihada za Marekani kusimamia mashauriano kati ya kundi la Taliban na serikali ya Afghanistan. Wachambuzi wa Taasisi ya Kimataifa kuhusu itikadi kali na machafuko ya kisiasa, wamebaini kuwa juhudi hizo zimeambulia patupu na wameelezea wasiwasi wao kama kweli hali hii inaweza kubadilishwa, ikizingatiwa Desemba mwaka ujao si mbali tena.

Vikwazo vya kufanya mazungumzo ni vingi na hakuna tarehe yoyote iliyopangwa kufanyaka mkutano wowote kwa wakati huu. Juhudi za hivi karibuni kujaribu kuishawishi serikali ya rais Hamid Karzai izungumze na Taliban zilishindikana mwezi uliopita kwa sababu ya upinzani wa rais huyo kuhusu alama iliyowekwa na Taliban nje ya makao yao makuu yaliyofunguliwa mjini Doha, nchini Qatar.

ARCHIV - Der afghanische Präsident Hamid Karsai (l)und US-Präsident Barack Obama (r)bei einer Pressekonferenz am 12.05.2010 im Weißen Haus in Washington. Eine Sammlung von 90 000 überwiegend geheimen Afghanistan-Militärdokumenten offenbart das Wiedererstarken der radikalislamischen Taliban im Krieg gegen die ISAF-Schutztruppe. Die US-Einheiten und deren Verbündete verlieren in dem seit knapp neun Jahren andauernden Krieg am Hindukusch zunehmend an Boden - ihre Sicherheitslage ist prekär. Sie verschlechtere sich auch im Norden des Landes, wo deutsche Soldaten im Einsatz sind. Die Protokolle sollen von der Enthüllungs-Website Wikileaks veröffentlicht werden. Die Dokumente belegen auch die Existenz einer US-Elitetruppe zur Liquidierung von Taliban-Anführern. EPA/MIKE THEILER +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais wa Marekani, Barack Obama na wa Afghanistan, Hamid KarzaiPicha: picture-alliance/dpa

Hata hivyo ripoti hiyo inaishutumu Marekani kwa kufanya makosa kadhaa ya kimkakati yaliyosababisha matatizo yanayoyakumba mazungumzo. Ryan Evans, mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo, alisema Jumatatu wiki hii wakati wa uzinduzi wake kuwa juhudi za Marekani kufanya mazungumzo zilifanyika wakati usiofaa; zilichelewa mno, hivyo kuupa mchakato huo muda mchache sana kuweza kuzaa matunda.

Frederic Grare, Mkurugenzi wa Mpango wa Asia Kusini katika shirika la Carnegie Endowment kwa ajili ya amani ya kimataifa, pia ana shaka shaka kama kutafanyika mazungumzo ya maana kati ya serikali ya Karzai na wanamgambo wa Taliban kabla majeshi ya Marekani kuondoka nchini Afghanistan mwaka ujao, akisema muda hauruhusu.

Sauti nyingi mno

Wakati huo huo, ripoti hiyo inaikosoa Marekani kwa kukosa sauti moja wakati inapozungumza na Waafghanistan na hivyo kutoa ishara za kukanganya kuhusu malengo yake. Inadokeza kuwa wanachama wa wakala za serikali ya Marekani, kama vile wizara ya ulinzi, wizara ya mambo ya kigeni na baraza la usalama wa kitaifa, zinafuatlia ajenda tofauti nchini Afghanistan.

Kwa upande mwingine wanamgambo wa Taliban nao hawana umoja kama inavyotakikana kuhakikisha mazungumzo yanakuwa ya maana. Lakini Marekani imejitia kitanzi yenyewe kwa kufanya kazi bila kulitilia maanani suala hili, ripoti hiyo inasema. Grare anajuta kwamba sauti muhimu zimeachwa nje ya mazungumzo. Anaamini kuyafukuza nje makundi mengine mbali na Taliban, rais Karzai alijiwekwa mwenyewe katika hali ya kutengwa.

Kämpfer der Taliban in Uruzgan in Afghanistan.
Wapiganaji wa TalibanPicha: picture alliance / Ton Koene

Kufanya kazi pamoja

Wataalamu wengine wanasisitiza Marekani haina chaguo lengine mbali na kushinikiza mazungumzo ya maana yafanyike kabla kuondoka majeshi ya kimataifa mwaka ujao. "Tunaweza kubakia Afghanistan hadi mwaka 2014 au 2024," amesema Bill Goodfellow, muasisi wa Taasisi ya sera za kimataifa mjini Washington, wakati alipozungumza na shirika la habari la IPS. Hadi tutakaposimamia mazungumzo yatakayofikia suluhu ya kisiasa, haitakuwa na maana yoyote," akaongeza kusema mtaalamu huyo. Goodfellow anasisitiza umuhimu wa kuyajumuisha mataifa na pande zote husika, ikiwemo Iran, taifa ambalo linazozana na Marekani.

Ripoti ya Taasisi ya Kimataifa ya masuala ya itikadi kali na machafuko ya kisiasa imewasilisha mapendekezo kadhaa inayosema huenda yakaziongeza fursa za Marekani kufikia makubaliano ya kugawana madaraka nchini Afghanistan kwa njia ya mazungumzo. Inaishauri Marekani kuzungumza kwa kauli moja, kwa mfano kwa kuwadhibiti wajumbe wote wa serikali yake walio nchini Afghanistan. Kwa kufanya kazi pamoja Marekani inaweza kuhakikisha Waafghanistan wanaelewa msimamo wake na lengo lake. Ripoti hiyo pia inapendekeza Marekani ihakikishe wadau wote wanashirikishwa katika mchakato huo na mahitaji ya jamii ya Waafghanistan yanatiliwa maanani.

Mwandishi: Josephat Charo/IPS

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman