1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMARAH: Utulivu warejea

21 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0Y

Hali ya utulivu imerejea mjini Amara, kusini mwa Irak kufuatia siku mbili za machafuko makubwa kati ya maofisa wa usalama wa serikali na wanamgambo wa madhehebu ya Shia.

Mapigano yalianza juzi Alhamisi baada ya polisi kumkamata mwanachama wa jeshi la Mahdi la shehe mwenye siasa kali, Moqtada al Sadr, na kumshitaki kwa kutega bomu lililomuua afisa wa ngazi ya juu wa idara ya ujasusi.

Wapiganaji wa jeshi la Mahdi walivivamia na kuvichoma moto vituo vya polisi hivyo kuzusha mapigano makali katika barabara za mji wa Amarah. Watu takriban 18 waliuwawa na wengine wasiopungua 100 walijeruhiwa katika mapigano hayo.

Inadhaniwa kwamba utulivu umerejea mjini Amarah kufuatia hatua ya Moqtada al Sadr kuwatolea mwito wafuasi wake waache kupigana na badala yake akawatuma wapambe wake mjini Amarah kuzungumza na polisi juu ya kuyasitisha mapigano.