1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMARAH: Wanamagambo wa Kishia wapambana na polisi

21 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0d

Nchini Irak,mapambano kati ya polisi na wafuasi wa kiongozi wa kidini wa Kishia,Moqtada al-Sadr yameua si chini ya watu 15 na wengine wapatao dazeni kadhaa wamejeruhiwa.Mapigano hayo yalizuka katika mji wa Amarah kusini mwa nchi baada ya mwanachama wa “Jeshi la Mahdi” la wanamgambo wa al-Sadr kukamatwa na polisi.Mtu huyo ameshukiwa kuhusika na mauaji ya polisi wa upelelezi kutoka eneo hilo.Kama wanajeshi 700 wa Kiiraki wamepelekwa mji huo kudhibiti mapigano na kusimamia amri ya kuwazuia watu kutoka nje,lakini haijulikani ikiwa sasa hali ya mambo imedhibitiwa.Vikosi vya Kingereza vilivyoikabidhi serikali ya Irak mji huo miezi miwili iliyopita, vimesema vimekaa tayari kuingia mji huo pindi itahitajika kufanya hivyo.