1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makubwa makubwa yaahidi kuajiri maelfu ya wakimbizi Ulaya

Iddi Ssessanga
19 Juni 2023

Makampuni makubwa ya kimataifa yakiwemo Amazon, Marriot na Hilton yameahidi Jumatatu kuajiri zaidi ya wakimbizi 13,000, wakiwemo wanawake wa Ukraine waliokimbia vita na Urusi, katika kipindi cha miaka ijayo barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/4Sld0
Amazon Prime Drohne
Picha: Amazon/AP/picture alliance

Kuelekea maadhimishi ya siku ya kimataifa ya wakimbizi Jumanne, zaidi ya mashirika 40 makubwa yamesema yataajiri, kuwaunganisha na kazi au kuwapa mafunzo jumla ya wakimbizi laki mbili na nusu, ambapo 13,680 kati yao wakipata ajira moja kwa moja katika mashirika hayo.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaeshughulikia wakimbizi Kelly Clements, alisema watu milioni 110 wamepoteza makazi yao kote duniani, huku takribani milioni 12 kati yao wakitokea Ukraine, na karibu nusu yao wanaishi Ulaya kufuatia wimbi kubwa zaidi la wakimbizi barani humo tangu vita kuu ya pili ya dunia.

Clements alisema kila idadi ni hadhiti ya familia binafsi iliyoacha kila kitu kutafuta usalama, ulinzi na kutaka kuwa na uwezo wa kujijenga upya haraka iwezekanavyo. "Hivyo ahadi za makampuni zilizotolewa Jumatatu ni muhimu sana", alisema.

Soma pia: Ujerumani yatafakari maombi wa uhamiaji nje ya Ulaya

Msumukumo wa kuajiri barani Ulaya uliandaliwa na shirika lisilo la faida la Tent Partnership for Refugees, lililoasisiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Chobani, Hamdi Ulukaya, linaloziunganisha biashara na wakimbizi, na umezinduliwa wakati wa mkusanyiko mjini Paris.

Mkutano wa kwanza wa kundi hilo uliofanyiaka nchini Marekani ulipelekea ahadi za kuajiri wakimbizi 22,725.

Amazon kuajiri wakimbizi 5,000

ROMANIA-UKRAINE-RUSSIA-CONFLICT
Wakimbizi wa Ukraine wakiwa kwenye kambi baada ya kuvuka mpaka wa nchi hiyo na Romania, Aprili 14, 2022. Makampuni makubwa yameahidi kutoa ajira kwa wakimbizi zaidi ya 13,000 barani Ulaya.Picha: AFP via Getty Images

Katika duru hii mpya, kampuni ya duka la mtandaoni ya Amazon inaongoza, ikiahidi kuajiri wakimbizi wasiopungua 5,000 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo barani Ualya, ikifuatia na Marriot na Hilton ziliuoahidi kuajiri wakimbizi 1,500 kila mmoja, huku Starbucks na ISS zikiahidi kajiri wakimbizi 1,000 kila mmoja na ahadi ndogo ndogo kutoka kampuni kama vile Adidas, L'Oreal, PepsiCo na Hyatt.

Makamu wa rais wa kampuni ya Amazon Ofori Agboka anaesimamia rasilimali watu, alisema mpango huo ni mzuri kwa kampuni yao kwa sababu fursa ya kuongeza utofauti kwenye safu ya wafanyakazi itandelea kuifanya kuwa kampuni imara, na kuongeza kuwa utofauti unaleta ubunifu pamoja na mitazamo tofauti.

Soma pia: Umoja wa Mataifa wa ripoti ongozeko la vifo vya wakimbizi wanaovuka bahari ya Mediterian.

Amazon ilitangaza kupunguza nafasi 27,000 za kazi mapema mwaka huu, kama sehemu ya wimbi la upunguzaji, baada ya kampuni hiyo ya teknolojia kuajiri watu wengi wakati wa janga la Uviko-19.

Daria Sedhi-Volchenko alikimbia Kyiv mwaka uliopita na sasa anafanya kazini mjini Warsaw, Poland kama meneja programu mwandamizi katika programu ya huduma za wavuti ya Amazon inayotoa mafunzo ya bure kwa wa Ukraine. Anasema asilimia 40 ya waliomo kwenye programu hiyo hawana ujuzi wa masuala ya teknolojia.

Kampuni zinatumai kuwa wakimbizi wanaweza kujaza mahitaji ya wafanyakazi baada ya uchumi kufufuka tena kutokana na athari za janga. Barani Ulaya, ukosefu wa ajira uko katika kiwango chake cha chini kabisaa tangu kuanzishwa kwa sarafu ya euro mnamo mwaka 1999.

USA New York, Brooklyn | Jobmesse für Flüchtlinge aus der Ukraine
Wakimbizi wa Ukraine wakihudhuria maonyesho ya ajira mjini Brooklyn, New York, Marekani, Februari 1, 2023.Picha: Andrew Kelly/REUTERS

Changamoto za wakimbizi

"Tunashuhudia rekodi ya ongezeko la mahitaji katika hoteli zetu katika masoko mengi hapa Ulaya", alisema mtendaji mkuu wa kampuni ya Marriot International Anthony Capuano. Na hivyo sasa wanaajiri pakubwa ili kuhakikisha wanaweza kuwahifadhi wageni kadiri mahtaji yanapoongezeka.

Soma pia: Mataifa ya Magharibi yaendelea kuisaka suluhu mzozo Ukraine

Mataifa ya Ulaya yamewakaribisha wa Ukraine, na wakati naibu katibuu Clements amesifu hatua ya kufungua shule, maeneo ya kazi na fursa nyingine kwa ajili yao, alisema fursa sawa na hizo zinapaswa kutolewa kwa wengine wanaokimbia mizozo na migogoro katika maeneo kama Syria, Sudan na Afghanistan.

Sedihi-Volchenko anazijua changamoto zilizoko mbele ya wakimbizi, hata wakati baadhi ya kampuni zinatoa msaada wa ujuzi wa lugha, ushauri nasaha na mafunzo. Orodha za kazi zinaweza kuwa ngumu kufumbua, na kama yeye, wanaweza kukabiliwa na ugumu katika kupata mtandao imara wa intaneti au nguo za kazi.

Chanzo: AP