1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amerika ya Kaskazini kushuhudia kupatwa kamili kwa jua

Lilian Mtono
8 Aprili 2024

Mamilioni ya watu katika eneo kubwa la Amerika ya Kaskazini watashuhudia hii leo kupatwa kwa jua, wakati ambapo mwezi utalifunika kabisa jua kwa zaidi ya dakika nne katika baadhi ya maeneo.

https://p.dw.com/p/4eXLr
Sonnenfinsternis
Picha: NASA/IMAGO/USA TODAY Network

Tukio hilo litashuhudiwa ikiwa hali ya hewa itaruhusu na linatarajiwa kuanzia Mexico, kupitia Marekani hadi Canada.

Wanaofurahia tukio kama hili tayari wamekusanyika katika maeneo ambako kutatokea kupatwa kamili kwa jua, ikiwa ni pamoja na kwenye mji wa Fredericksburg, katikati mwa jimbo la Texas, ambako linatarajiwa kutokea muda mfupi baada ya saa 7.30 mchana.

Tukio hili la dakika 4 na sekunde 28 litadumu kwa muda mrefu zaidi ya la mwaka 2017 lililodumu kwa dakika 2 na sekunde 42. Kulingana na shirika la utafiti wa masuala ya anga za mbali la Marekani,NASA, kupatwa kamili kwa jua kunaweza kudumu kuanzia sekunde 30 hadi karibu dakika 7 na nusu.