1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMMAN: Mtoto wa kike wa Saddam ajitokeza kwenye maandamano

2 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdx

Mtoto wa kike wa Saddam Hussein aliye uhamishoni nchini Jordan, alijitokeza kwa muda mfupi kwenye maandamano yaliyofanywa jana mjini Amman. Raghad Saddam Hussein aliwashukuru mamia ya waislamu wa madhehebu ya Sunni walioshiriki katika maandamano hayo na kumtaja babake aliyenyongwa juzi Jumamosi, kuwa shahidi.

Wakati haya yakiarifiwa, serikali ya Irak imeanza kuchunguza vipi walinzi walivyompiga picha Saddam Husein wakati alipokuwa akinyongwa. Picha hizo zimekugeuza kunyongwa kwa Saddam kuwa maonyesho ya runinga ambayo yamezusha hasira za kikabila nchini Irak.

Afisa wa ngazi ya juu serikalini ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba balozi wa Marekani nchini Irak alijaribu kumshawishi waziri mkuu Nuri al-Maliki asiharakishe kumnyonga Saddam Hussein siku nne baada ya ombi lake kukataliwa na badala yake akaitaka serikali isubiri kwa muda wa wiki mbili.

Habari za kifo cha Saddam na jinsi alivyotendewa na viongozi wa serikali kulisababisha mgomo katika jela moja kwenye eneo la Wasunni karibu na mji wa kaskazini wa Mosul.