1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMMAN:Mfalme Abdullah ampongeza Bush

17 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhn

Mfalme Abdullah wa pili wa Jordan amepongeza hatua ya Rais George Bush wa Marekani kuitisha mkutano wa kimataifa kusaka amani mashariki ya kati, akisema kuwa hiyo ni hatua maridhawa.

Katika hotuba yake jana usiku, Rais Bush alipendekeza kufanyika kwa mkutano huo kwa nia ya kufufua mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina.

Rais Bush aliahidi tena nia yake ya kutaka kuona suluhisho linapatikana katika mzozo wa mataifa hayo mawili ya Israel na Palestina.