1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty International lashtumu jeshi la Ethiopia kwa mauaji Somalia

24 Aprili 2008

-

https://p.dw.com/p/Dnet

ADDIS ABABA

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limewashutumu wanajeshi wa Ethiopia kwa kuwateka nyara watoto 40 wakisomali wakati wa walipofanya uvamizi katika msikiti mmoja wiki iliyopita.Shirika hilo limetaka kuachiliwa huru kwa watoto hao.Aidha shirika hilo limelaani mauaji ya zaidi ya watu 20 wakiwemo wanazuoni wakati wa uvamizi huo.Hata hivyo jeshi la Ethiopia limekanusha kuhusika na mauji hayo ya raia wasio na hatia wakati wa mapigano yao makali na waasi.

Mkurugenzi wa shirika hilo lenye mako yake mjini London Uingereza Kate Allen amelitaka baraza la usalama la Umoja wa mataifa kufanya uchunguzi juu ya kukiukwa kwa haki za binadamu katika ghasia nchini Somalia.

Waziri mkuu wa Somalia Nur Hassan Hussein pia ametetea serikali yake na wanajeshi wa Ethiopia kuhusu suala hilo na kusema walikuwa wakijikinga dhidi ya kushambuliwa katika mapigano ya mwishoni mwa juma.Watu zaidi ya 20 walikutwa wamechinjwa kinyama ndani ya msikiti mjini Mogadishu mwishoni mwa juma.