1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amri ya kukamatwa Al Bashir

Oumilkher Hamidou29 Machi 2009

Muendesha mashtaka mkuu ataka Al Bashir atengwe

https://p.dw.com/p/HM97

Berlin:


Muendesha mashtaka mkuu wa korti ya uhalifu ya kimataifa,Luis Moreno-Ocampo amewahimiza viongozi wa jumuia ya kimataifa washirikiane katika kuchukua hatua dhidi ya rais Omar al-Bashir wa Sudan."Hiyo ndiyo njia pekee ya kumaliza mauwaji ya halaiki huko Darfour na kufuatwa amri ya kimataifa ya kumkamata Al Bashir" amesema Moreno-Ocampo,katika mahojiano pamoja na gazeti la "Das Parlament".Muendesha mashtaka mkuu wa korti ya kimataifa ya uhalifu ametoa mwito rais wa Sudan atengwe na jumuia ya kimataifa ili Sudan ikubali kumtoa.Bwana Luis Moreno-Ocampo ameongeza kusema watu milioni mbili na nusu wanakufa kidogo kidogo katika jimbo la Darfour.