1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMSTERDAM: Chama cha Christian Demokratik chapata ushindi katika uchaguzi wa bunge nchini Uholanzi

23 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqE

Chama cha Christian Demokratik cha waziri mkuu wa Uholanzi, Jan Peter Balkenende, kimepata ushindi katika uchaguzi wa bunge uliofanyika hapo jana. Christian Demokratiks wamepata viti 41 juu ya 150 vinavyounda baraza la wawakilishi katika bunge la nchi hiyo. Chama muhimu cha upinzani cha Leba kimepata viti 32. Chama cha tatu ni chama cha socialist ambacho kimepata viti 26. Chama hicho kiliambulia viti 9 tu katika uchaguzi wa mwaka 2003.

Kutokana na kusambaratisha kura na uungwaji mkono unaozidi kupanda kwa makundi madogo madogo ya kisiasa, wadadisi wa mambo ya kisiasa wanasema kutaendelezwa uundwaji wa serikali ya muungano.

Kampeni kubwa ya uchaguzi ilitwama juu ya swala la uhamiaji, lakini waziri mkuu, Balkenende, alisisitiza juu ya kuinuka uchumi wakati wa mhula wake.