1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMSTERDAM: Kesi ya watuhumiwa wa ugaidi 6 imeanza nchini Uholanzi

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD27

Kesi ya raia wa Uholanzi 6 wanaotuhumiwa kuhusika na ugaidi, imeanza kuskilizwa jana mjini Amsterdam. Kundi hilo la watu 6, wanatuhumiwa kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi, kwa jina Hofstad Group, ambalo linatuhumiwa kupanga mauaji ya wanasiasa mashuhuri na mashambulizi kwenye majengo ya serikali.

Wendeshamashtaka wamesema wamekusanya ushahidi dhidi ya watuhumiwa hao ambao walikamatwa wakiwa na silaha na nyaraka zinazoelezea namna ya kuweza kuripua bomu kwa kutumia simu za mkononi. Mmoja wa watuhumiwa hao mwenye asili ya Morokko, Samir Azzouz, alikamatwa na polisi kufuatia kuuliwa mtungafilamu mashuhuri, Theo van Gogh, mwaka wa 2004.