1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMSTERDAM: Vyama vyashauriana kwa faragha kuhusu kuunda serikali ya muungano.

3 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdb

Mashauriano yanaendelea nchini Uholanzi ili kuunda serikali ya muungano.

Chama cha mrengo wa kushoto cha Waziri Mkuu wa muda Jan Peter Balkenende kinaendesha mashauriano ya faragha na chama cha Labour na chama kingine kidogo cha kidini.

Jaribio la kwanza la kuunda serikali ya mseto liligonga mwamba mwezi Novemba baada ya vyama husika kukosa kukubaliana kuhusu sera.