1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amsterdam.Kesi ya watuhumiwa wa ugaidi yaanza nchini Uholanzi.

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD21

Kesi ya Wa-Holanzi sita wanaotuhumiwa kuwa ni wanachama wa kundi la kigaidi imeanza mjini Amsterdam.

Kundi hilo linatuhumiwa kuwa na muingiliano na kundi linaloitwa Hoftad na linalaumiwa kwa kupanga mashambulizi dhidi ya wanasiasa na majengo ya seriklai.

Waendesha mashtaka wa uholanzi wamesema kuwa, tayari wameshakusanya ushahidi wa wazi na hivi sasa wanaweza kutumia sheria ngumu katika kujaribu kujaribu kusadikisha makosa yao.

Watuhumiwa walikutikana wakiwa na silaha za kisasa na za kizamani, zinazoelezea jinsi ya kuweza kuripua kwa kutumia simu za mikononi.

Mmoja kati ya mtuhumiwa ni Muholanzi mwenye asili ya Moroco, Samir Azzouz, alikuwa wa kwanza kukamatwa na polisi kufuatia mauaji ya mtengenezeji filamu Theo van Gogh mnamo mwaka 2004.