1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ancelotti ana imani Benzema na Modric watasalia Real Madrid

7 Aprili 2023

Kocha wa timu ya kandanda ya Uhispania ya Real Madrid Carlo Ancelotti amesema hii leo kuwa ana imani wachezaji Karim Benzema, Luka Modric na Toni Kroos watasalia katika timu hiyo msimu ujao.

https://p.dw.com/p/4Pp3u
European Super Cup - Real Madrid v Eintracht Frankfurt
Picha: Kai Pfaffenbach/Reuters

Watatu hao wanamaliza mkataba wao mwishoni mwa msimu huu na Ancelotti amethibitisha kuwa Modric na Kroos kwa sasa wanazungumza na klabu ya Real Madrid kuhusu mustakabali wao.

Benzema alijiunga na  Real Madrid  kutoka Lyon mwaka wa 2009 na Modric aliwasili kutoka Tottenham mwaka 2012, wawili hao mbali na mataji mengine, wameshinda mara tano Ligi ya Mabingwa wakiwa na Real Madrid.

Toni Kroos alijiunga na Real Madrid akitokea Bayern Munich mwaka 2014, na kushinda Champions League mara nne akiwa na timu hiyo ya Real Madrid inayoitwa pia Los Blancos.