1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uturuki imeondoa pingamizi.

Abdu Said Mtullya4 Aprili 2009

Jumuiya ya kijeshi ya NATO imepata katibu mkuu mpya. Waziri mkuu wa Denmark

https://p.dw.com/p/HQFe
Waziri mkuu wa Denmark Anders Fogh Rasmussen amechaguliwa kuwa katibu mkuu mpya wa NATO.Picha: AP

STRASBOURG.

Viongozi wa NATO wamekubaliana kumchagua waziri mkuu wa   Denmark ,kuwa katibu mkuu mpya  wa jumuiya yao.

Televisheni ya Denmark imeripoti kuwa bwana Anders Fogh  Rasmussen amechaguliwa baada  ya viongozi wengine wa NATO kufanikiwa kuishawishi Uturuki.

Hapo awali Uturuki ilimpinga waziri mkuu huyo kwa  sababu ya jinsi alivyoshughulikia mzozo juu ya kukashfiwa mtume wa dini ya kiislamu Muhammad katika vyombo vya habari nchini  Denmark.

Katibu mkuu  wa  hadi  sasa  Jaap  de Hoop Scheffer atajiuzulu mwishoni mwa mwezi julai.