1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Angela Merkel katika Umoja wa Mataifa

26 Septemba 2007

Kanzela wa Ujerumani ameitaka Iran ithibitishe haiundi bomu la atomiki na akasema Ujerumani itayari kukalia kiti katika Baraza la Usalama. Rais wa Iran Ahemdinejad hakuregeza nae kamba .Ametetea haki ya nchi yake ya kutumia ufundi wa kinuklia.

https://p.dw.com/p/CB0y
Picha: AP

Katika hotuba yake ya kwanza kabisa mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani aliitisha jana msimamo mkali dhidi ya mradi wa Iran wa kinuklia.

Nae Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran, ameitetea mbel ya Baraza hilo haki ya nchi yake ya kutumia ufundi wa kinuklia kwa matuimizi ya amani.

Baraza la Usalama limeidhinisha nalo kutumwa kwa vikosi vya UM nchini Chad na Jamhuri ya Afrika ya kati kuwalinda wakimbizi kutoka Dafur.

Wakati mawaziri wa nje wa Marekani,Russia,China,Uingereza,Ufaransa na Ujerumani wanatazamiwa kukutaka leo pembezoni mwa kikao cha Baraza Kuu la UM kujadiliana jinsi gani ya kuitia shindo zaidi Iran,iachane na mradi wake wa kinuklia,Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani,aliitisha UM ufanyiwe marekebisho na hasa Baraza la Usalama la Umoja huo.Alisema,

“Katika umbo lake la sasa,Baraza la Usalama halimuriki sura ya ulimwengu ilivyo hii leo.Kwahivyo, hakuna njia nyengine baraza hilo lijirekebishe ili lilingane na ukweli wa hali ya mambo ulivyo leo.

Ujerumani imechangia mno mnamo miaka iliopita katika mjadala wa marekebisho hayo.Ujerumani itayari hata kuchukua mojawapo wa viti vya kudumu katika Baraza hilo la Usalama.”

Alisema Bibi Angela Merkel.

Kuhusu haja ya kuchukuliwa hatua madhubuti kupambana na uchafuzi wa mazingira kabla kumalizika kwa mapatano ya sasa ya Kyoto,Kanzela Merkel alisema:

“Haikuwahi kabla wanasayansi kukubaliana kama hivi sasa juu ya dhara zinazochafua hali ya hewa,ukweli uko wazi,haja ya kuchuliwa hatua haikataliki.Kila nchi inaathirika na mabadiliko ya hali ya hewa na hakuna awezae peke yake kupambana na balaa hilo.”

Kuhusu Iran, kanzela wa Ujerumani alidai na ninamnukulu,”Si dunia ithibitishe,bali Iran yenyewe inapaswa kuthibitisha kuwa haina nia ya kuunda bomu la atomiki.”

Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran katika hotuba yake mbele ya Baraza hilo kuu la UM alitilia nguvu haki ya nchi yake kutumia ufundi wa kinuklia kwa madhumuni ya amani.

Akaukataa kwa mara nyengine tena mwito unaoitaka Iran isimamishe mradi wake wa kurutubisha madini ya uranium akidai Iran kamwe haitapiga magoti kuitikia amri dola zisizo na uhalali na za kijeuri.Hapo tena, rais wa Iran akautangaza mzozo wa mradi wake wa kinuklia na Jumuiya ya kimataifa umemalizika.Alisema sasa uko mikononi mwa Shirika la UM la nguvu za atomiki.

Baraza la Usalama la UM limeidhinisha nalo kikosi cha Umoja wa Ulaya na kikosi cha polisi cha UM kupelekwa Chad na Jamhuri ya Afrika ya kati ili kuwalinda wakimbizi kutoka mkoa wa Dafur,nchini Sudan.

Kuhusu mada hii, rais George Bush wa Marekani ambae jana pia alihutubia kikao cha baraza kuu kabla rais wa Iran, alisema:

Baraza kuu la UM linaendelea na kikao chake.