1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ankara. Kansela anafuturu na waziri mkuu Ankara.

5 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5r

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amewasili katika mji mkuu wa Uturuki Ankara, ambako anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan na maafisa wengine.

Miongoni mwa mambo mengine , kansela anatarajiwa kuzungumzia nia ya Uturuki kutaka kujiunga na umoja wa Ulaya.

Akizungumza na gazeti linalosomwa na watu wengi nchini Ujerumani, la Bild, Merkel amesema ni muhimu kwa Uturuki kutimiza majukumu yake na kutekeleza kwa ukamilifu masharti ya uanachama wa umoja huo.

Amesema kuwa kutatua mzozo na Cyprus ni muhimu kwa ajili ya uhusiano kati ya nchi hiyo na umoja wa Ulaya.