1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Shambulio la bomu lilifanywa na mwanamgambo wa kikurdi

23 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBz6

Wachunguzi wa shambulio la jana la bomu lililowaua watu sita mjini Ankara lilifanywa kutumia mbinu zinazotumiwa na kundi la waasi wa kikurdi.

Gavana wa mji wa Ankara, Kemal Onal, amemtaja mshambuliaji wa jana wa kujitoa mhanga maisha kuwa Guven Akkus, mwanamume wa miaka 28 aliyetumikia kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kubandika mabango yasiyo halali na kupingana na polisi wakati wa maandamano ya sikukuu ya wafanyakazi ambayo mara kwa mara hukumbwa na machafuko nchini Uturuki.

Hata hivyo gavana Onal hakutaja aina za mabango au ikiwa mshambuliaji huyo ana uhusiano na kundi la waasi lililojitenga la Wakurdi, Kurdistan Workers Party, PKK.

Gavana huyo amesema mwili wa Akkus ulitawanyika vipande vipande wakati wa mlipuko uliotokea kwenye kituo cha basi mbele ya duka kubwa mjini Ankara.

Rais wa Urusi Vladamir Putin amelitaja shambulio la jana mjini Ankara kuwa ushahidi wa kuhuzunisha kwamba ipo haja ya kuongeza juhudi za kupambana na ugaidi duniani.