1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Uturuki bado yadinda kuitambua Cyprus

5 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBum

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank -Walter Steinmier ameeleza masikitiko yake kuhusu Uturuki kushindwa kuchukua hatua za kuitambua Cyprus.

Katika ziara yake nchini Uturuki bwana Steinmier amesema kuwa amesikitishwa kuwa serikali mjini Ankara haijatekeleza hatua hii ikiwa ni miongoni mwa mapendekezo iliyotakiwa kuyatimiza ili kujiunga na umoja wa ulaya.

Umoja wa ulaya pia unaishinikiza Uturuki kufanya mageuzi zaidi kuelekea katika demokrasia.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmier alizuru mji mkuu wa Ankara ukiwa ni wajibu wa Ujerumani kama mwenyekiti wa sasa wa nchi wanachama wa umoja ulaya.