1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Uturuki haitoshambulia wanamgambo kaskazini mwa Iraq

12 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsL

Waziri Mkuu wa Uturuki,Recep Tayyip Erdogan amefutilia mbali kuchukuliwa kwa hatua ya kijeshi dhidi ya wanamgambo wa Kikurd kaskazini mwa Iraq. Alipozungumza na waandishi wa habari kabla ya mkutano wa usalama wa ngazi ya juu,Erdogan alisisitiza kuwa hatua za kijeshi ziwe za mwisho kuchukuliwa.Akaongezea kuwa Ankara inashughulika kupambana na waasi walio katika ardhi ya Uturuki. Lakini wakuu wa kijeshi wamesema,operesheni upande wa pili wa mpaka inahitajiwa ili kuvishinikiza vituo vya chama cha PKK cha Wakurd, kilichopigwa marufuku nchini Uturuki.Baghdad na Washington zinapinga kabisa hatua yo yote ile ya Uturuki kuingia kaskazini mwa Iraq.