1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Uturuki yaimarisha harakati za kijeshi mpakani

27 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CD

Waziri Mkuu wa Uturuki,Recep Tayyip Erdogan amezituhumu nchi za Umoja wa Ulaya kuwa hazisaidi kupambana na waasi wa Kikurd.Amesema,wafuasi wa chama cha Kikurd cha PKK kilichotiwa katika kundi la magaidi,wanajificha nchi za Umoja wa Ulaya bila ya shida.Uturuki mara kwa mara,imezitaka nchi za Umoja wa Ulaya kuchukua hatua dhidi ya wanamgambo wa PKK na makundi mengine ya Kituruki yaliyopigwa marufuku.

Kwa upande mwingine,maafisa wa Uturuki na Irak waliokutana siku ya Ijumaa mjini Ankara, wameshindwa kuafikiana njia ya kupambana na waasi wa Kikurd wanaoishambulia Uturuki kutoka kaskazini mwa Irak.Sasa Uturuki inaimarisha harakati zake za kijeshi katika eneo linalopakana na Irak ya Kaskazini.