1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA : Waandamana kupinga Erdogan kuwania urais

15 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9r

Katika mji mkuu wa Uturuki Ankara hapo jana watu 200,000 wamendamana dhidi ya mipango ya Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan kugombania urais wa nchi hiyo mwezi ujao.

Waandamanaji wanahofu kwamba Erdogan ambaye alikuwa Muislamu wa siasa kali hapo zamani anaweza kutumia madaraka kutekeleza agenda ya Kiislamu.Uturuki ni taifa lisiloambatana na misingi ya kidini ijapokuwa kwamba ni nchi ya Kiislam.

Kwa upande wake Erdogan ameushutumu uongozi wa Umoja wa Ulaya wa Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.Gazeti la kila wiki nchini Ujerumani la Spiegel limemkariri waziri mkuu huyo wa Uturuki akikuita kushindwa kwa Ujerumani kuialika Uturuki kusheherekea miaka 50 ya Umoja wa Ulaya kuwa ni kosa kubwa.

Kiongozi huyo wa Uturuki anatarajiwa kuwasili mjini Berlin leo hii kwa mazungumzo na Kansela huyo wa Ujerumani.