1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Washukiwa ugaidi wamekamatwa Uturuki

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCl3

Polisi nchini Uturuki wanasema wamekamata idadi fulani ya watu wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda.Mmoja kati ya hao waliokamatwa ni mwanasheria mwenye miaka 25 na aliesema kuwa yeye ni kiongozi wa kundi hilo nchini Uturuki.Washukiwa hao,walikamatwa katika operesheni zilizofanywa wakati mmoja katika mji mkuu Ankara,Istanbul na mji wa magharibi wa Izmir.Katika siku za nyuma,wanamgambo wa Al-Qaeda wamelaumiwa kuhusika na mashambulio kadhaa yaliyoilenga Uturuki.