1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA:Gul aidhinisha Baraza la mawaziri

30 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUa

Rais mpya wa Uturuki Abdullah Gul ameidhinisha baraza la mawaziri lililopendekezwa na waziri mkuu Recep Tayyip Ardogan ambaye ni mshirika wake.

Baraza hilo linajumuisha vigogo mbalimbali wenye historia tofauti ya kuwa na misimamo ya kiislamu pamoja na isiyopendelea utawala kwa misingi ya kidini.

Aliyekuwa waziri wa uchumi Ali Babacan anayepigania Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya amechukua wadhifa wa waziri wa mambo ya nje uliokuwa unashikiliwa na bwana Gul.

Wapinzani wa Gul wanasema watamfuatilia kwa karibu rais huyo mpya kuona ikiwa ataonyesha upendeleo wowote kuegemea serikali inayoelekea kuwa ya kiislamu.