1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ankara:Kura ya maoni juu ya marekebisho ya katiba.

21 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Dv

Kura ya maoni inafanyika leo nchini Uturuki, kuamua iwapo rais awe akichaguliwa moja kwa moja na raia badala ya bunge. Chama tawala cha AKP cha waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan, kimewataka wapiga kura waunge mkono mabadiliko hayo yaliopendekezwa, ambayo ni pamoja na kupunguza kipindi cha rais hadi miaka mitano na kupunguza kipindi cha bunge kutoka miaka mitano hadi minne. Mabadiliko hayo hayatamgusa rais wa sasa Abdullah Gul aliyechaguliwa na bunge mwezi Agosti , kwa kipindi cha miaka saba .