1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA:Rasimu ya mabadiliko ya uteuzi wa rais yawasilishwa bungeni

4 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7IZ

Chama tawala nchini Uturuki kimewasilisha rasimu ya mabadiliko ya katiba bungeni yanayolenga kuondoa uwezekano wa mabishano ya kisheria katika kipindi cha miaka 7 ya utawala wa Rais Gul.Mabadiliko hayo yanadhaniwa kuwa muhimu huku chama tawala cha AKP kinasubiriwa kufanya kura ya maoni tarehe 21 mwezi huu.

Moja ya mabadiliko hayo inapendekeza rais kuchaguliwa na umma badala ya kuteuliwa na bunge.Kulingana na wataalam wa kisheria na vyama vya upinzani mapendekezo hayo huenda yakamlazimu Rais Gul aliyeingia madarakani mwezi Agosti kushiriki tena katika uchaguzi mkuu katika kipindi cha siku 40.

Mapendekezo ya chama cha AKP huenda yakamwezesha Rais Gul kutoshiriki katika uchaguzi huo na kumaliza muhula wake kwanza.Ila huenda yakatimizwa na mrithi wake.

Chama cha AKP kiliitisha uchaguzi wa mapema mwezi Julai na kupata ushindi mkubwa jambo lililomwezesha Bwana Gul kuteuliwa tena mwezi uliofuatia.