1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA:Recep Tayyip Erdorgan ameshinda uchaguzi wa bunge

23 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfx

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayip Erdogan ambae ameshinda uchaguzi uliomalizika, sasa amejiuzulu ili atoe nafasi ya kuombwa upya kuunda serikali.

Matokeo ya uchaguzi wa bunge wa mwishoni mwa wiki nchini Uturuki yameonyesha ushindi mkubwa wa chama cha AKP cha waziri mkuu Recepp Tayyip Erdogan.

Chama cha AK kimepata asilimia 47 huku chama cha Republican Peoples kikiwa na asilimia 21 na chama cha National Movement kimefanikiwa kupata zaidi ya asilimia 10 zinazohitajika ili kuweza kuwakilisha bungeni.

Wakosoaji wa chama cha AKP wameelezea wasiwasi wao kwamba ushindi wa chama cha hicho utadidimiza nia ya Uturuki ya kupambana na utawala wenye misingi ya kidini, hata hivyo waziri mkuu Erdogan ameapa kuwa atazingatia katiba inayo tenganisha dini na dola, pia amesema kuwa ataendeleza juhudi za Uturuki kutaka kujiunga na Umoja wa Ulaya.