1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA:Uturuki kuanzisha operesheni ya kijeshi ya waasi wa Kikurdi

10 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7H7

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameliidhinisha jeshi la nchi hiyo kuanzisha operesheni katika eneo la mpaka wake na Irak dhidi ya kundi la waasi wa Kikurdi.

Hatua hiyo imefuatia mkutano kati ya waziri mkuu bwana Erdogan na maafisa wa ngazi za juu katika jeshi la Uturuki mjini Ankara.

Taarifa ya serikali ya Uturuki imesema kwamba hatua zote ikiwemo ile ya kutekeleza operesheni ya kijeshi zitachukuliwa dhidi ya makundi ya kigaidi.

Matamshi hayo yanatafthiriwa kuwa Uturuki inataka kupambana na kundi la waasi wa Kikurdi la PKK ambao inaaminika kuwa walihusika na mauaji ya wanajeshi 15 wa Uturuki yaliyotokea mwishoni mwa wiki.

Msemaji wa serikali ya Uturuki bwana Ali Al Dabbagh amesema, hatua ya kijeshi sio suluhisho na wala haitaangamiza harakati za kundi lililopigwa marufuku la PKK dhidi ya serikali ya Uturuki.

Bwana Al Dabbagh amesema nchi yake inaamini kuwa ushirikiano wa pande mbili Irak na Uturuki au wa pande tatu pamoja na Marekani utawezesha kufaulu kulishinda kundi hilo la waasi la PKK.