1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Annan akutana na Assad

10 Machi 2012

Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa na mataifa ya Kiarabu Kofi Annan akutana na rais Bashar al-Assad kutoa msukumo kwa ajili ya kuwapo kwa suluhisho la kisiasa nchini humo.

https://p.dw.com/p/14Iab
In this photo released by Insider Images for UN Foundation , former United Nations Secretary-General and UN Foundation Board member Kofi Annan, addresses the 'New African Connections' conference hosted in Oslo, Norway, by NORAD, CARE, and supported by the UN Foundation, Tuesday, June 21, 2011. The UN Foundation Board meeting in Norway includes discussions which focus on ways to help new partners connect with the lifesaving work of the United Nations. (AP Photo / Stuart Ramson/Insider Images for UN Foundation, HO) NO SALES NORWAY OUT
Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa na mataifa ya Kiarabu Kofi AnnanPicha: dapd

Mazungumzo ya Annan mjini Damascus yanakuja siku moja baada ya wanaharakati kusema kuwa majeshi ya utawala wa rais Assad yamewauwa watu 68 wakati yakijaribu kupanua udhibiti wao dhidi ya mji wenye uasi wa Homs na kuzima upinzani wa kundi la watu wenye silaha katika jimbo la kaskazini la Idlib.

Arab League kukutana

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa ya Kiarabu pia wanatarajiwa kuwa na mazungumzo mjini Cairo na waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov. Urusi na China zilipiga kura ya veto dhidi ya mswada wa umoja wa mataifa mwezi uliopita ambao ungeunga mkono mpango wa umoja wa mataifa ya Kiarabu unaotaka Assad kujiuzulu.

Wanaharakati wamesema kuwa makombora yaliyofyatuliwa kutoka katika vifaru pamoja na mabomu kadha yameanguka katika wilaya zinazoshikiliwa na wapinzani katika mji wa Homs, na kuuwa watu 20, ambapo 24 wameuwawa katika jimbo jirani la Idlib na vifo zaidi vimeripotiwa kwingineko.

epa03126550 An undated handout photograph made available by the Local Coordination Committes (LCC) in Syria on 29 February 2012, shows syrian armoured vehicles at a street in the suburb of Damascus, Syria. According to media reports on 29 February, Syrian government forces were set to launch a new attack on the restive province of Homs. The move came as overnight the United Nations put the total death toll from 11 months of conflict in the country at well over 7,500. EPA/LOCAL COORDINATION COMMITTES LCC HANDOUT BEST QUALITY AVAILABLE. EPA IS USING AN IMAGE FORM AN ALTERNATIVE SOURCE, THEREFORE EPA COULD NOT CONFIRM THE EXACT DATE AND SOURCE OF THE IMAGE HANDOUT EDITORIAL USE ONLY/NO SALES +++(c) dpa - Bildfunk+++
Majeshi ya Syria yakiwa na vifaru katika mji wa HomsPicha: picture-alliance/dpa

Vifaru 30 viliingia katika kitongoji chetu asubuhi ya leo na wanafyatua makombora katika nyumba, amesema Karam Abu rabea, mkaazi wa kitongoji cha Karm al-Zeitoun katika mji wa Homs.

Urusi yatakiwa kusaidia

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Rodham Clinton siku ya Ijumaa amesema kuwa ana matumaini mkutano wa Urusi na umoja wa mataifa ya Kiarabu mwishoni mwa juma hili utasaidia kuileta Urusi katika mstari kuhusiana na mzozo wa Syria.

Akiziita juhudi kuhusu Urusi kuwa ni zenye uzito mkubwa , Clinton amewaambia waandishi habari katika wizara ya mambo ya kigeni kuwa amezungumza na waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov mapema wiki hii, juu ya kile alichokiita, "matumaini yetu kuwa Urusi itachukua jukumu muhimu katika kumaliza mauaji na kufanyakazi kuelekea katika kipindi cha mpito cha kisiasa nchini Syria.

U.S. Secretary of State Hillary Rodham Clinton speaks during a meeting with Japanese Foreign Minister Koichiro Gemba, not pictured, at the State Department in Washington, Monday, Dec. 19, 2011. (AP Photo/Luis M. Alvarez)
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Rodham ClintonPicha: AP

Amesema kuwa atafuatilia siku ya jumatatu mjini New York , wakati atakapoonana na Lavrov katika majadiliano ya ngazi ya juu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa juu ya maendeleo tangu kuzuka kwa vuguvugu la mageuzi katika mataifa ya Kiarabu.

zaidi ya watu 7,500 wameuwawa katika mzozo huo ambao umeanza mwaka mmoja uliopita.

Mwandishi : Sekione Kitojo / dpae/rtre

Mhariri: Bruce Amani.