1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANSUNCION : Rais wa zamani gerezani miaka 8 kwa ubadhirifu

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmU

Rais wa zamani wa Paraguay Luis Gonzales Macchi hapo jana amehukumiwa kifungo cha miaka minane gerezani kwa ubadhirifu wa mali ya umma wakati akiwa madarakani.

Macchi ambaye aliiongoza Paraguay kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2003 ametozwa faini ya dola 450,000.Mahkama katika mji mkuu wa Ancuncion pia imetaifisha dola 360,000 kutoka akiba ya siri ya Macchi kwenye benki ya Zurich.

Macchi alisisitiza kwamba zaidi ya dola milioni moja zilizokutikana kwenye benki ya Zurich hapo mwaka 2003 alikuwa ameachiliwa na bibi yake lakini mahkama imesema ameshindwa kuthibitisha madai yake hayo.

Mahkama imeamuru kukamatwa mara moja kwa Macchi ambaye amesema atakata rufaa kupinga hukumu hiyo.